Miss International Tanzania 2025, Faidha Kassie, ambaye pia ni mwakilishi wa Miss Grand, ameondoka jana kuelekea nchini Misri kushiriki mashindano ya kimataifa ya Miss Grand International.
Faidha anaenda kuiwakilisha Tanzania kwa fahari mbele ya dunia, akibeba ndoto, utamaduni na uzuri wa Mtanzania katika jukwaa la kimataifa. Kabla ya kuondoka, amewaomba Watanzania kumpa sapoti kwa kumpigia kura kwa kufuata maelekezo yanayotolewa kupitia.
Ushiriki wake ni fursa muhimu ya kulitangaza taifa kimataifa, na sapoti ya Watanzania itakuwa mchango mkubwa katika safari yake ya ushindi.