Nyota wa Real Madrid, Vinícius Júnior, ameripotiwa kuamua kutochapisha ujumbe wowote wa kumuaga Xabi Alonso kwenye mitandao yake ya kijamii, hatua iliyozua gumzo kubwa miongoni mwa mashabiki.
Kwa mujibu wa taarifa zinazosambaa, Vini Jr anadaiwa kuwa miongoni mwa wachezaji watatu waliopinga baadhi ya mawazo na falsafa za kiufundi za Xabi Alonso alipokuwa akihusishwa na mradi wa timu hiyo.
Wachezaji waliotajwa katika ripoti hizo ni:Vinícius Júnior,Jude Bellingham na Federico Valverde
Inaelezwa kuwa wachezaji hao hawakuwa na uhusiano mzuri na mbinu za Alonso, jambo ambalo huenda lilichangia hali ya sintofahamu ndani ya kikosi na ukosefu wa mshikamano wa kiufundi.
Uamuzi wa Vini Jr kukaa kimya kwenye mitandao ya kijamii, tofauti na ilivyozoeleka kwa wachezaji kutoa ujumbe wa shukrani au kuaga makocha, umechukuliwa na wengi kama ishara ya wazi ya kutokuwepo kwa uhusiano mazuri kati yake na kocha huyo Mhispania.
Hadi sasa, hakuna kauli rasmi kutoka kwa Vini Jr wala Real Madrid kuthibitisha madai hayo, lakini sakata hilo linaendelea kuibua mjadala mkubwa kuhusu nguvu ya wachezaji wakubwa na changamoto za utekelezaji wa falsafa mpya za ukocha katika klabu yenye presha kubwa kama Real Madrid