Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Tanzania inaendelea kuwa na imani kuwa mazungumzo na ushirikiano ni muhimu kukabiliana na changamoto za Dunia.
Rais Dkt Samia amesema hayo katika halfa ya kufungua mwaka mpya 2026 na mabalozi wanaowakilisha nchi zao, namashirika ya kimataifa hapa nchini leo Ikulu ya Chamwino Dodoma.
Amesema dunia inakabiliwa na changamoto za Migogoro, kuyumba kwa Uchumi, na mabadiriko ya Tabia nchi na kwamba kwa dunia hii mazungumzo yanaweza kuwa suluhu kwa changamoto zinazo ikabili Dunia.
Aidha, Rais Samia amesema hafla ya leo ni ishara ya dhamira ya Tanzania kuimarisha diplomasia na ushirikiano wa kimataifa kwa maslahi ya taifa na amani ya dunia.
Hata hivyo Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki Balozi Mahmoud Thabit Kombo, amesema maandamano yaliyosababisha Vurugu wakati na baada yauchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Oct. 29-31 2025 yalisababisha uharibifu wa mali za Umma na Binafsi hali iliyo chafua Taswira ya nchi Kimataifa.
Amesema kuwa hali hiyo ilisababisha hata baadhi ya fedha kutoka mataifa mengine duniani kwa ajli ya tanzania kuzuiliwa na kukosekana kwa uhakika wa Kiuchumi.
Hali aliyoitaja kuwa ni ngumu kwasbabu matukio hayo yametokea kwa mara ya kwanza baada ya miaka 64 ya Uhuru.