Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia Denis Ogesa (28), mkazi wa Nairobi nchini Kenya, kwa tuhuma za kuvunja, kuingia na kuiba fedha katika benki ya Azania, tawi la Namanga wilayani Longido.
Ogesa anadaiwa kukamatwa wakati akiendelea kutekeleza tukio hilo la kihalifu katika benki hiyo ambapo alikamatwa akiwa tayari na Sh91.28 milioni pamoja na fedha za Kenya, Sh288,700.
Kwa mujibu wa taarifa kwa umma, iliyotolewa usiku wa leo Jumatano Januari 14, 2026 na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo imedai mtuhumiwa huyo alikamatwa usiku wa kuamkia leo saa 6:40 usiku.
“Mtuhumiwa wakati akiendelea kutekeleza tukio la kihalifu katika benki hiyo alikamatwa akiwa tayari na fedha za Tanzania, Sh91.28 milioni na fedha za Kenya, Sh 288,700,” imedai taarifa hiyo na kuongeza
“Jeshi la Polisi linakamilisha uchunguzi wa watu alioshirikiana nao ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.”