Staa wa Senegal, Sadio Mane, amemshukuru mchezaji wa Misri, Mohamed Salah, pamoja na taifa lake kwa kuonyesha ushindani wa hali ya juu, baada ya ushindi wa Senegal kupelekea timu yao kufuzu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
Mane alisema kwamba anamheshimu sana Salah na anathamini mchango wake mkubwa kwenye soka la Afrika.
Senegal iliibuka na ushindi wa gori moja(01) dhidi ya Misri na sasa timu ya Senegal itachuana na wenyeji wa michuano hiyo Morroco kwenye fainali za AFCON.