Mwenyekiti wa CHAN na AFCON kutoka Tanzania, na Mkurugenzi wa Mto Mawe ,Madam Rona Lymo amewasili nchini usiku wa kuamkia leo Jan 16, 2026 akitokea Morocco.
Akizungumza na Waandishi wa Habari amesema kuwa Fursa zitakazopatikana kwenye Mashindano ya Afcon mwaka kesho (2027) ambapo Tanzania itakuwa ni moja ya wenyeji wa Mashindano hayo ni Fursa ambazo kila Mtanzania anauwezo wa kuzichangamkia akitolea mfano Morocco ambao ndio wenyeji Mwaka huu Wananchi wake walivyochangamkia.
Pia kubwa zaidi alilokuja nalo ni kushiriki maandalizi ya Tuzo za Serengeti Awards, ambapo kampuni yake ya Mto Mawe imeingia kwenye kiny’ang’anyiro cha Best Attraction (Private Owned).