Jukwaa la Matumaini
Siku moja baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi huo, Museveni amesema matokeo hayo yameonyesha uthabiti wa chama chake kinachojulikana kama National Resistance Movement.
Katika hotuba yake hiyo, Museveni pia ameushtumu upinzani kwa kujaribu kuzua vurugu wakati wa upigaji kura, na kuwataka viongozi wa dini kuwashauri vijana ambao huenda wanapotoshwa kuzua vurugu.
Museveni amesema baadhi ya wapinzani wamekosea huku akimtaja mpinzani wake wa karibu Bobi Wine na wengine kama wasaliti.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa pongezi kwa Rais Mteule wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni, aliyeibuka ushindi katika uchaguzi uliofanyika nchini humo wiki iliyopita.
Rais Samia ametoa pongezi hizo kupitia chapito katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.