Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala Ndogo ya Dar es salaam imepanga Januari 23, 2025 kuanza kusikiliza maombi ya kibali cha kuishtaki Serikali ambayo yamefunguliwa na Waziri wa zamani, Geoffrey Mwambe.
Uamuzi huo umetolewa hii leo Januari 20, 2026 ambapo Mwambe alifungua Kesi hiyo iliyopewa namba 488 ya mwaka 2026 dhidi ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji na Mwanasheria Mkuu wa Serikali baada ya kupokonywa Passport yake na ya familia yake yenye watu watano.
Nje ya Mahakama Wakili wa Mwambe, Hekima Mwasipu amezungumza na vyombo vya habari kuhusu kesi hiyo.