Marekani imejiondoa rasmi katika Ushirikiano wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), hatua ambayo inafanya nchi hiyo kutokuwa mwanachama wa shirika hilo kwa mara ya kwanza tangu ilipojiunga kama mwanachama mwanzilishi mwaka 1948.
Taarifa ya pamoja iliyotolewa jana Alhamisi, Januari 22, 2026 na Waziri wa Afya wa Marekani, Robert F. Kennedy Jr, pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje, Marco Rubio, imethibitisha kukamilika kwa taratibu za kuiondoka Marekani WHO.
Sababu kuu ya uamuzi huo wa Marekani imetaja kuwa ni mapungufu ya shirika hilo wakati wa janga la COVID-19 huku wakisema pia michango yote ya kifedha kwa WHO imesitishwa.