Baada ya karibu mwezi mmoja wa ukimya, Abigail Chams amerudi kwenye Instagram na video ya kumgusa kila aliyemsikia.
Badala ya kurudi na Reels za fashion au teaser za studio, labda na wimbo mpya, Abigail ameanza upya kwenye mizizi ya imani, iliko asili ya muziki wake (kabla ya umaarufu wa kwenye Bongo Fleva), akiimba Tenzi Namba 144 “Mbele Ninaendelea” huku akipiga piano, moja ya ala tano za muziki anazozimudu.
Video hiyo imekubaliwa na mashabiki waliommwagia sifa, wengine wakiweka wazi hisia za kuguswa kwao na uimbaji huo “Daah… umetugusa sana ”