Mashabiki wa Bongo Fleva wanashuhudia kile tunachoweza kusema kilisubiriwa kwa hamu, taarifa kwamba Alikiba na Mbosso wako studio wakijiandaa kuachia kolabo yao ya kwanza.
Wote hawa ni mastaa wakubwa wa muziki wa Tanzania, kila mmoja akijulikana kwa ubunifu wake: Mbosso kwa maandishi yenye hisia na ustadi wa kuigiza maneno, na Alikiba kwa melodies zinazokaa moyoni mwa mashabiki, hali inayoongeza matarajio kwamba kolabo hii inaweza kuibuka kama mojawapo ya ngoma kubwa za mwaka 2026.
Ingawa wimbo huu bado haujatbulishwa rasmi, tunatarajia kwamba ushirikiano huu utavuka mipaka ya Tanzania na kuibuka kama wimbo unaoburudisha Afrika Mashariki na zaidi. Ni wazi kwamba iwapo Alikiba na Mbosso watawekeza nguvu kwenye promo, wimbo huu unaweza kuwa moja ya ngoma zinazozungumzwa zaidi mwaka huu.