
Mashabiki wa muziki wamekaribisha remix ya wimbo wa“All My Enemies Are Suffering” ambao ni wa Bien kutoka Kenya na Phyno wa Nigeria
Remix hii imeunganisha midundo ya Afrobeat, huku sauti ya hisia za @bienaimesol zikikamilisha nguvu ya mistari ya rap ya Phyno, Wimbo huu pia umeingiza midundo ya Isikuti, ikichangia asili ya Kiafrika na kuunganisha jamii mbali mbali za Afrika kupitia muziki.
Mashabiki wamekaribisha wimbo huu kwa shangwe, ukipata maelfu ya wasikilizaaji ndani ya siku zake za kwanza huku wengi wanapongeza jinsi sauti za wasanii wote zilivyochanganyika kwa ubunifu, ingawa wachache walisema wimbo wa kwanza ulikuwa tayari ni hit, na kuhoji umuhimu wa remix.
Pamoja na hiyo, Bien amekuwa akishirikiana moja kwa moja na mashabiki wake, akiendelea kuongeza hamasa kuhusiana na wimbo huu.
Remix hii inapatikana kwenye majukwaa makubwa ya muziki kama Spotify na Apple Music, ikiruhusu mashabiki wa duniani kote kufurahia ushirikiano huu wa mashariki na magharibi ya Afrika.
Wimbo huu ulitoka Septemba 10, 2025, na kuleta uhai mpya kwenye toleo la Julai 18, lililomhusisha Bien pekee.