Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikilia askari wa Jeshi la Magereza mwenye umri wa miaka 31 kwa tuhuma za kumuua mke wake, Betia Chacha, mkazi wa Ibadakuli, kwa kumkata na kipande cha chupa katika maeneo mbalimbali ya mwili.
Tukio hilo limetokea Novemba 30, 2025, na limethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi, ambaye amesema marehemu alikatwa kwenye mkono, shingo na mapaja, na kusababisha kifo chake papo hapo.
Kamanda Magomi amesema chanzo cha tukio hilo inadaiwa ni wivu wa kimapenzi na migogoro ya kifamilia,
Kamanda Magomi amewataka wananchi kuepuka kujichukulia sheria mikononi,na kusisitiza kwamba katika kipindi hiki cha Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia, Jeshi la Polisi linaungana na taasisi nyingine kupiga vita ukatili, hasa dhidi ya wanawake na watoto.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwa uchunguzi zaidi na mtuhumiwa anashikiliwa kwa hatua za kisheria.