David Mwaluseke

David Mwaluseke ni mtangazaji aliyebobea katika vipindi mbalimbali vya kijamii, burudani pamoja na jamii kwa ujumla. Pia ni mbunifu wa mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutengeneza matangazo na sauti yenye mvuto katika masikio ya walio wengi ambao wamekuwa wakifurahishwa anavyokuwa katika vipindi kadhaa.