
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania Jiji la Arusha limeanzisha kampeni ya kukabiliana na mmomonyoko wa maadili kwa vijana kwa kuviwezesha vituo vya kufundisha na kuhifadhi Quraan kutoa elimu ya maadili.
Akizungumza kwenye muendelezo wa kampeni hiyo katika kituo cha Allfurqaan Welfare Trust Katibu wa Bakwata Jiji la Arusha Sheikh Banka Seif amesema malezi ya watoto yanahitaji ushirikiano wa jamii katika ngazi zote kuanzia ndani ya familia.
Shikh Seifu amekabidhi vitabu vya mafundisho ya dini kwa yatima na wanaoishi Mazingira magumu kilichopo Kisongo kama njia ya kusaidia kuwalea vijana kwenye maadili mema yenye hofu na Mungu na raia wema.
Juhudi za kurejesha maadili mema kwa jamii zimekuwa zikifanywa na Serikali kwa kushirikiana na Mashirika na asasi za kiraia kukabiliana na mmmonyoko wa maadili unaotokana na Utandawazi.