
Moja ya kauli maarufu zaidi katika historia ya utamaduni wa burudani ya “I don’t know her” imeibuka tena katika mazungumzo ya mitandaoni na kwenye televisheni.
Kauli hiyo ilitolewa na Mariah Carey mwaka 2003 alipoulizwa kuhusu Jennifer Lopez kwenye mahojiano ili atoe maoni yake kuhusu Lopez, ambaye vyombo vya habari walikuwa wakimchukulia kama mpinzani wake wa moja kwa moja, Mariah alitabasamu, akatikisa kichwa kidogo, na akajibu kwa utulivu: “I don’t know her.”
Kauli hiyo iliwashangaza wengi, ikachukuliwa kama kejeli, huku mashabiki na mastaa waliitumia kama njia ya kuonyesha kutojali au kukwepa mivutano.
Kwa sasa, “I don’t know her” si tu kauli ya utani, bali imekuwa sehemu ya historia ya burudani inapotajwa, inakumbusha zama za mapambano ya mastaa, mvuto wa media, na jinsi meme culture inavyoweza kuunda urithi wa kisanii.
Mashabiki wengi wanaona kuwa kauli hii inawakilisha ubabe wa kimyakimya wa Mariah Carey, huku wengine wakiitumia kuonyesha hali ya kutojali kwa ustaarabu