
Rapa kutoka Nigeria, Emeka Akumefule maarufu Blaqbonez, ameibua mada ngumu mitandaoni baada ya kuelezea mtazamo wake tofauti kuhusu ndoa na uaminifu.
Msanii huyo wa lebo ya Chocolate City amesema hana tatizo kuwa na ndoa ya wazi, akieleza kuwa hamu ya kimwili kwenye uhusiano hupungua kadri muda unavyosogea.
Amefafanua kuwa kwake, uaminifu wa kihisia na uhusiano wa karibu wa kiakili vina thamani zaidi kuliko uaminifu wa kimwili. Anaamini hakuna mwanaume mwingine anayeweza kuvunja uhusiano wa kihisia atakaojenga na mke wake.
Kauli hiyo imezua mjadala mkubwa mitandaoni, mashabiki wakigawanyika kuhusu mtazamo wake wa ndoa za wazi na uhusiano wa kisasa.