
Serikali kupitia benki kuu ya Taifa BoT imesema itaendelea kununua dhahabu kutoka kwa wachimbaji wa madini kwa bei iliyopo katika ushindani wa dunia ili kutoa faida kwa wachimbaji
Rehema Kassim kutoka idara ya masoko ya fedha BoT amesema hayo mbele ya waziri mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa alipotembelea banda la benki hiyo katika maonesho ya nane ya madini mkoani Geita
Amesema serikali kwa mwaka 2024 mwezi oktoba benki hiyo iliwweka mkakati wa ununuzi wa dhahabu lengo likiwa ni kuwapa fursa wachimbaji kutunza dhahabu kwenye benki hiyo kwa mjibu wa sheria ya madini kifungu cha 59 sura ya 123 ambacho kinaelekeza kila mwenye leseni ya uchimbaji na mchimbaji auze angalau asilimia 20 ya mzigo wake kwenye benki hiyo
Amesema anayeuzia mzigo wake BoT anapata punguzo la malipo katika mrahaba ambapo awali ilikuwa aslimia 6 na sasa ni aslimia 4 na malipo ya ada ilikuwa asilimia moja na kwa sasa ni asilimia 0 na muuzaji anaweza pia kuiuzia BoT asilimia 100 ya mzigo wake kupitia kwenye viwanda vya uchenjuaji wa dhahabu ambavyoni ni Geita Gold Refinery Ltd (GGR), Mwanza Preciuos Metals co.Ltd pamoja na Eyes of Africa kilichopo Dodoma
Awali meneja mahusiano BoT Vicky Msina amesema BoT inahifadhi kinga ya fedha za kigeni kupitia ununuzi wa dhahabu ambayo inaisaidia nchi kuhifadhi fedha za kigeni kupitia hazina ya dhahabu
BoT ni moja ya taasisi amabazo zimeweza kutoa udhamini wa ujenzi wa mabanda 9 ya kudumu katika viwanja hivyo vya maonesho mkoani Geita
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa amehitimisha kwa kuzitaka taasisi za kifedha chini ya BoT pamoja na wadau wengine wa madini kuendelea kuonyesha uwepo wao katika kuihudumuia jamii hasa katika kuboresha miundombinu ya viwanja vya maonesho