Chama cha CNL nchini Burundi kimesema kuwa kina wasiwasi wa ongezeko la wafanyakazi wa serikali wanaoacha ajira zao na kwenda kutafuta kazi nje ya nchi.
Msemaji wa chama hicho Bw. Terrance Manirambona amesema hali hiyo inasababisha taifa kupoteza nguvu kazi muhimu akieleza kuwa wanaoacha kazi wanatoka katika sekta mbalimbali za umma.
Bw Manilambona amesema miongoni watumishi wa Umma wanaoacha kazi ni wahudumu wa Afya, walimu na watumishi wengine wa serikali hiyo ambao mchango wao ni muhimu kwa maendeleo ya jamii na Taifa.
Bw. Manirambona ameiomba serikali ya Burundi kuchukua hatua za haraka dhidi ya suala hilo akisema linaweza kukwamisha utekelezaji wa dira ya taifa ya kufikia uchumi wa kati ifikapo 2040–na nchi inayojitegemea mwaka 2060.