
KENYA: Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limetoa adhabu ya kupunguzwa kwa idadi ya mashabiki katika Uwanja wa Moi Kasarani uliopo Nairobi, Kenya kutokana na kujirudia kwa matukio ya vurugu yanayovunja kanuni za ulinzi na usalama viwanjani katika fainali za CHAN 2024 zinazoendelea.
Barua ambayo CAF imeandika kwa mwenyekiti wa Kamati ya Ndani ya maandalizi (LOC) ya Kenya imeijulisha nchi hiyo kuwa kuanzia sasa, Uwanja wa Moi Kasarani utakuwa unaingiza asilimia 60 tu ambayo ni sawa na mashabiki 27,000 ambayo ni tofauti na idadi kamili ya mashabiki ambayo Uwanja huo inaweza kuhimili ambao ni 48,000.
CAF imeanika sababu za kuchukua uamuzi huo ambazo imesema kuwa ni uvunjwaji wa kanuni za ulinzi na usalama za shirikisho hilo.