
Na, Fred Seleli
Mwanza
Mjumbe wa kamati ya ushindi wa Chama Cha Mapindunzi CCM jijini Mwanza, Kasibethi Joseph Ametoa wito kwa vijana kujihusisha katika uzalishaji ili waweze kujikuza kiuchumi.
Amesema hayo aliposhiriki katika mafunzo ya maadili kwa vijana yaliyofanyika katika kanisha la EAGT Malimbe nakuwataka vijana kuwa mbali na baadhi ya viongozi wanao watumia vijana kwa ajili ya masilai yao.
Aidha Kasibethi Joseph amesema vijana ndio taifa la kesho litakalo Saidia katika kudumisha amani ya taifa, Pamoja na kukuza maendeleo ya taifa kwa ujumla
Baadhi ya vijana walioshiriki katika mafunzo hayo wamesema wapo tayari kushiriki katika maendeleo Pamoja na kutotumika katika kuhatarisha amani ya nchi….