
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche amewataka wananchama na wananchi kwa ujumla kupuuza taarifa za kuwa chama hicho kimegawanyika.
Heche ameyasema hayo leo Mei 23, 2025 alipozungumza muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha kamati kuu ya chama hicho, kinachofanyika Makao Makuu ya Chadema, Mikocheni jijini Dar es Salaam kilichoanza leo na kuhitimishwa kesho.
Ameongeza kuwa wanaoondoka ni wachache ikilinganishwa na idadi ya wajumbe wa vyombo vya uamuzi vya chama.
Aidha Heche amesisitiza kuwa ajenda yao ya No Reforms no Election wanaendelea nayo kwa kuwa ina ukweli kuhusu chaguzi kutowatendea haki wagombea wao.