
Majirani wa nyumba ya Hollywood Hills wameripoti kuwa msanii D4vd (David Anthony Burke, 20) na msichana aliyepotea Celeste Rivas (15) walikuwa wakikaa pamoja nyumbani hapo.
Taarifa hii imetolewa huku polisi wakiwa bado wanaendelea na uchunguzi na kukusanya ushahidi kutokana na mwili wa Celeste kupatikana ndani ya Tesla ya msanii huyo.
Mmoja wa majirani amesema aliporudi Los Angeles wiki hii baada ya safari, alishangazwa sana na taarifa hiyo na kwamba walikuwa kimya sana na hakuwahi kuona polisi pale, wala kusikia wanasherehekea au kufanya sherehe yoyote, hakukuwa na kitu chochote cha ajabu.
Celeste Rivas alipotoweka zaidi ya mwaka mmoja uliopita kutoka nyumbani kwa mama yake, na polisi wanaamini alikuwa akiwa na D4vd hadi mwili wake kuonekana ndani ya Tesla hiyo. Uchunguzi unaendelea huku mashabiki na wadau wa muziki wakiwa na mshangao mkubwa.