Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limemchagua mbunge wa Babati Vijijini Bw. Daniel Sillo kuwa Naibu Spika wa Bunge kwa asilimia mia moja.
Uchaguzi wa Sillo umefanyika leo November 13, 2025 kwa kupata kura 371 akiwa ndi mgombea pekee wa nafasi ya Naibu Spika muda mfupi baada ya kuthibitishwa kwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ameomba ushirikiano kutoka kwa wabunge wa bunge hilo.
Sillo amechukua nafasi iliyoshikiliwa na Mussa Azzan Zungu katika Bunge la 12 ambaye kwa sasa ni Spika wa Bunge la Tanzania akipokea Kiti hicho kutoka kwa Dkt. Tulia Akson aliyejiondoa kwenye mchakato wa kuwania nafasi hiyo.
Kabla ya wadhifa huo, Sillo amewahi kushika nafasi mbalimbali kama Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti.