
Mtendaji Mkuu Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Mohamed Besta amesema usanifu uliofanywa na makisio yake kwa Daraja la JP Magufuli, daraja hilo litaishi zaidi ya miaka 100.
Mhandisi Besta ameyasema hayo leo wakati wa mahojiano Maalumu na waandishi wa habari kuelekea uzinduzi rasmi wa daraja hilo uliofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan leo hii.
Amesema kuwa ili liwezi kudumukwa muda mrefu baada ya kuzinduliwa na magari kuanza kulitumia wanaweka mpango maalumu wa usimamizi wa matengenezo ya daraja hilo chini ya TANROADS yenyewe.
Rais Samia Suluhu Hassan amezindua Daraja la JP Magufuli Kigongo-Busisi lenye urefu wa kilomita 3.0 na barabara unganishi yenye urefu wa kilometa 1.66 Mchana huu jijini Mwanza.