
Mwanamuziki Davido kutoka nchini Nigeria amechaguliwa kuwa miongoni mwa wanachama wa GrammyAwards ambao wanaweza kupiga kura kwa kuteua wasanii gani wagombee katika vipengele gani pamoja na wasanii wapi wanafaa kushinda tuzo tofauti.
Recording Academy hupokea wanachama kutoka idara mbalimbali za muziki kama vile wasanii, watayarishaji na waandishi wa nyimbo ili kuhakikisha upigaji kura unahusisha wataalamu wa tasnia.
Davido ameeleza kufurahishwa na hatua hiyo ambayo ameipiga na kuongeza kuwa amefurahi kuona kilio chake na kilio cha wasanii wa Afrika kimesikika kwa maana ya kupata mwakilishi sahihi katika jukwaa hilo.