Watumishi wa umma wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera wametakiwa kutoa huduma kwa wananchi kwa kuzingatia sheria na mikataba ya mwajiri wao kuondoa Migongano.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Biharamulo SACP Advera Bulimba wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri hiyo ikiwa ni hatua ya kuwakumbusha wajibu wao kwa wananchi.
Amesema chini ya Uongozi wake serikali haita sita kuchukua hatua za kinidhamu kwa watumishi ambao wanashindwa kuwajibika kwa wananchi na kushindwa kusimamia miradi ya maendeleo na kukaa maofisini.
Baadhi ya washiriki wa kikao hicho wameahidi kufanya kazi kwa bidii na kuwajibika kwa wananchi kwa kadili watakavyohitaji huduma kutoka kwao na kusimamia miradi ya maendeleo katika maeneo yao.