
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Dkt. Kedmon E. Mapana, amempongeza mwandaaji wa Tuzo za Best Brand Afrika 2025, Ndg. Zakayo Shushu, kwa jitihada zake za kuenzi makampuni yanayojitahidi kukuza biashara zao kwa weledi na kujulikana kwa umma.
Dkt. Mapana amesema hayo wakati wa kilele cha hafla zilizofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, mbele ya wageni waalikwa kutoka sekta mbalimbali.
Kwa upande wake, mwandaaji wa tuzo hizo, Ndg. Zakayo Shushu, amesema amejisikia faraja kuona mwitikio mkubwa na kuheshimu makampuni yaliyofanya vizuri ndani na nje ya Afrika kwa kutunukiwa tuzo za heshima.
Shushu ameongeza kuwa mwakani wamepanga mikakati kabambe, kwani lengo lao ni kueneza tuzo hizi zaidi Afrika, kuanzia nyumbani Tanzania na hatimaye katika nchi zote za bara.
Usiku huo, taasisi na makampuni mbalimbali yalibeba tuzo, huku pia wakiwashukuru watu binafsi waliyochangia kwenye sekta mbalimbali za sanaa, serikali, na biashara.