Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewataka Watanzania kulinda, kuimarisha na kudumisha Muungano wa Tanzania, amani, utulivu na umoja wa kitaifa kama msingi wa maendeleo endelevu.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 02 Aprili , 2026 wakati wa uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026 uliofanyika Uwanja wa Gombani, Pemba.

Aidha, Rais Mwinyi amesema taasisi zote nchini na wananchi kwa ujumla wana wajibu wa kuheshimu utu, haki, usawa na utawala wa sheria ili kuendeleza mshikamano wa Taifa.
Mwenge wa Uhuru umeanza mbio zake katika Mkoa wa Kusini Pemba na unatarajiwa kufikia kilele chake Oktoba 14, 2026 mkoani Rukwa, ukiwa na kaulimbiu: “Tanzania ni Yetu Sote, Tushikamane.”

