
Chama cha Mapinduzi CCM kimekabidhi eneo lenye ukubwa wa ekari 10 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya kata ya Ulowa Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga
Akizungumza wakati wa kukabidhi eneo hilo kwa niaba ya Katibu mkuu wa CCM Dkt. Emmanuel Nchimbi, Katibu wa chama hicho Wilaya ya Kahama Andrew Chatwanga amesema chama hicho kimetoa eneo hilo ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya chama hicho ya mwaka 2020 inayolenga kuboresha huduma za jamii hasa sekta ya afya
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ushetu Emanuel Cherehani amesema tayari fedha za ujenzi shilingi Milioni 500 zimekwishatolewa na Serikali na hivyo ujenzi unatarajiwa kuanza mara moja
Kukamilika kwa kituo hicho cha afya kutawakomboa ziadi ya wananchi 36,000 ambao kipindi kirefu wamekuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata matibabu katika kituo cha afya cha kata jirani ya Ushetu