Mchekeshaji wa Kenya, Eric Omondi ametangaza nia ya kuwania nafasi ya kisiasa kama Mwakilishi wa Vijana katika Uchaguzi Mkuu wa 2027.
Akizungumza leo, Omondi alisema ushiriki wa vijana kupitia kura ni muhimu kwa kubadilisha mustakabali wa Kenya akidai vijana wanapaswa kushika uongozi na akafichua mipango ya kushinikiza mabadiliko makubwa ya kikatiba baada ya uchaguzi, yakiwemo kupunguza idadi ya kaunti na kuondoa baadhi ya nyadhifa za kuchaguliwa.
Aidha, alikosoa viongozi kwa kuwadharau vijana, akisema matukio ya hivi majuzi yanaonyesha dhana potofu dhidi yao.