
Serikali imesema itawachukulia hatua kali za kisheria watoto wote ambao watashindwa kuwatunza,kuwadharau na kuwafanyia ukatili wazazi wao ambao wameshafikia hatua ya uzee.
Naibu Waziri Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Mwanaidi Hamisi amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Moshi Vijijini, Profesa Patrick Ndakidemi aliyetaka kujua ni lini serikali itatunga Sheria yakumtaka mtoto kuwatunza wazazi wake
Katika swali la msingi, Profesa Ndakidemi ameuliza ni kwa nini Serikali isione haja ya kulazimisha watoto badala ya kuweka tamko peke yake na kupanua wigo kwa watoa huduma.
Naibu Waziri Mwanaid Kahamis amesema Serikali itaendelea kuwalea na kuwapatia matunzo wazee wasiojiweza ambao hawana familia na ndugu wa kuwatunza kupitia makazi ya wazee na wasiojiweza 13 inayoyamiliki.