
Rapa Fid Q ametangaza kwa furaha kubwa kwamba wimbo wake mpya “GLORY 2”, aliyoshirikiana na Damian Soul na Jose Chameleon, umeidhinishwa na kuzingatiwa katika mchakato wa tuzo za 68 za Grammy.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, @therealfidq amesema “Hii sio ushindi wangu tu—ni wa SISI. 💯 Kutoka Tanzania 🇹🇿 hadi Uganda 🇺🇬 na dunia nzima tunaunda historia pamoja!”
Fid Q pia alitumia nafasi hiyo kutoa shukrani kwa wale wote waliokuwa sehemu ya mradi huo, wakiwemo @@tashstam, @igloo_ent , @the_blackv1rus, @tazgoemi ambaye ni mtayarishaji wa wimbo huo, @slimsal_daresalim, @_shucxy_tz_, @HunterNatio, na @AYtanzania!
Msanii huyo ameweka wazi kuwa yote ni kwa heshima ya Mungu, ameongeza ameweka imani yake kwa mungu na sifa zote.
Wimbo huu ni sehemu ya Albamu ya #KitaaReJex iliyotolewa Agosti 13, 2025.