Wimbo wa “God Design” wa Jux kwa ushirikiano na Phyno, umeandika historia mpya ndani ya miezi sita tu tangu kutolewa baada ya kuvuka streams zaidi ya milioni 5 kwenye Spotify, hatua kubwa inayouweka wimbo huu kwenye daraja la juu la muziki wa Afrika Mashariki kwenye majukwaa ya kimataifa.
Kutoka Mei 2025 hadi sasa, God Design imekuwa miongoni mwa nyimbo zinazokua kwa kasi ya ajabu, ikipenya playlists za mataifa mbalimbali na kuonesha ukubwa wa ushawishi wa Jux kama mmoja wa wasanii wanaoongoza kwa ubora wa R&B na Bongo Fleva.
Ukuaji huu wa streams ni ushahidi wa nguvu ya mashabiki, uzito wa production ya @foxxmadeit na brand ya @africanboy_hq ambayo imeendelea kujiimarisha ndani na nje ya Tanzania.
Kwa sasa, God Design ndio wimbo wa Bongo uliofanya vizuri zaidi kwenye Spotify mwaka 2025, ukizidi kuonesha jinsi muziki wa Tanzania unavyoendelea kufungua milango ya kimataifa.
Kwa mafanikio haya mapya, @juma_jux anaendelea kuthibitisha msimamo wake kama msanii anayejenga daraja kati ya Bongo Fleva ya nyumbani na masikio ya duniani.