Msanii wa “kibao Kata”, Bi. Halima Haji, amerejea tena kuomba msamaha kwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) baada ya kupewa adhabu ya kufungiwa kujihusisha na shughuli za sanaa kwa miaka mitatu pamoja na kutozwa faini ya shilingi milioni tatu.
Aidha, Bi. Halima Haji amemuomba pia msamaha Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima na jamii kwa ujumla, akieleza kuwa muziki wa “kibao Kata” ndio chanzo chake kikuu cha kipato na unamwezesha kumhudumia mwanae pamoja na mama yake.
Msanii huyo alipewa adhabu hiyo baada ya video yake kusambaa mitandaoni na kudaiwa kwenda kinyume na maadili ya Tanzania.
