
Serikali katika Halmashauri ya Wilaya ya Msalala imezindua rasmi chanjo kwa wanyama wa kufugwa (Ng’ombe, mbuzi, na kondo) likilenga kufikia ng’ombe laki 182,000 huku mbuzi na kondoo elfu 82,000 zikitarajiwa kufikiwa katika zoezi hilo litakalodumu kwa muda wa wiki tatu kuanzia agosti 25, 2025
Akizungumza na Radio kwizera Ofisa Mifugo Halmashauri ya Msalala Michael Martin amesema lengo la chanjo hiyo ni kuchanja mbuzi na kondoo ugonjwa wa SOTOKA ya mbuzi (PPR) na ng’ombe ugonjwa wa Homa ya mapafu (CBPP) ambao huambukizwa kwa njia ya hewa na ni hatari sanaa kutokana na miingiliano ya mifugo
Amesema kwa takribani saa mbili za siku ya ufunguzi wa chanjo hiyo wamefanikiwa kuchanja ng’ombe 1420 mbuzi na kondoo 508 na ikitarajiwa kuchanja zaidi ya ng’ombe 3000 kwa siku ya kwanza ya ufunguzi.
Mabula Bubinza ni miongoni mwa wananchi waliofika katika shughuli hiyo ya chanjo amesema kumekuwepo magonjwa mbalimbali kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi hivyo chanjo hiyo itaisaidia mifugo yao kuepuka magonjwa hayo yanayoweza kuchangiwa pia na mwingiliano wa wanyama.