
Katika kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa vyombo vya Habari kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025.
Kupitia mitandao ya kijamii Rais Samia ameandika kuwa “Ninaendelea kuvisihi vyombo vya habari kutumia weledi katika kazi zenu ili kuendelea kujenga na kuimarisha amani, utulivu na umoja wa kitaifa, hasa kipindi hiki tunapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu”
Aidha Rais Samia amesema Tanzania imepiga hatua katika kuimarisha Uhuru wa Vyombo vya Habari na kujieleza.
Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari huadhimishwa kila mwaka tarehe 3 Mei ambapo siku hii ilianzishwa na Umoja wa Mataifa mwaka 1993 kwa lengo la kukumbusha serikali wajibu wake wa kuheshimu na kulinda uhuru wa vyombo vya habari.
Aidha malengo mengine ni kuadhimisha misingi ya uhuru wa vyombo vya habari duniani, kuwatambua na kuwaenzi waandishi wa habari waliopoteza maisha yao wakitekeleza kazi yao na kukuza mazungumzo kuhusu changamoto na maendeleo ya vyombo vya habari.