
Papa Leo XIV ni shabiki mkubwa wa michezo, hasa tenisi na baseball.
Tenisi: Michezo Anayopenda na Kucheza
Papa Leo XIV, ambaye anajulikana kama Robert Francis Prevost, amejielezea kama mpenzi mkubwa wa tenisi na katika moja ya mahojiano yake aliwahi kusema:
“Ninajiona kama mchezaji wa tenisi wa kiwango cha kati. Tangu nilipoondoka Peru, sijapata nafasi nyingi za kucheza, kwa hiyo ninatarajia kurudi uwanjani (akacheka).”
Alipokuwa akihudumu kama askofu huko Peru, alijenga mapenzi ya dhati kwa mchezo huu, na hata baada ya kuchaguliwa kuwa Papa, bado ana hamu ya kuendelea kucheza tenisi.
Baseball: Shabiki wa Chicago White Sox
Kama mzaliwa wa Chicago, Papa Leo XIV ni shabiki wa muda mrefu wa timu ya Chicago White Sox ya Major League Baseball. Ingawa kuna taarifa zimedai baada ya yeye kuchaguliwa kuwa Papa ni shabiki wa Chicago Cubs, Lakini kaka yake alikanusha hilo na kusema:
“Hakuwa shabiki wa Cubs hata kidogo. Alikuwa shabiki wa Sox kila wakati.”

Mapenzi yake kwa White Sox yamekuwa ya kudumu, ambapo katika moja ya mechi za fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2005 alihudhuria akiwa amevaa jezi ya timu hiyo.
Soka: Mfuasi wa Alianza Lima
Wakati akihudumu nchini Peru, Papa Leo XIV alikua mfuasi wa timu ya soka ya Alianza Lima, moja ya vilabu maarufu zaidi nchini humo. Mapenzi yake kwa timu hii yalijengwa wakati wa huduma yake ya muda mrefu kama askofu huko Chiclayo.
Kwa hivyo, Papa Leo XIV ni shabiki wa kweli wa michezo, akionesha mapenzi yake kwa tenisi, baseball, na soka.