Msanii chipukizi wa Bongo Fleva, @itare.fr , ameachia rasmi EP yake mpya, kazi ambayo ameielezea kama hatua kubwa sana kwenye safari yake ya muziki.
Kupitia ujumbe wake mfululizo kwenye Instagram, Itaré aliwashukuru familia, marafiki, timu yake na mashabiki waliomfuatilia tangu enzi za freestyle kwenye gari hadi sasa anapopiga hatua za kitaalamu.
EP hiyo ina jumla ya nyimbo 7, zikiwemo kolabo za kimataifa na wasanii kutoka Tanzania,India, Nigeria na Afrika Kusini.
Tracklist ya EP ni kama ifuatavyo:1. Snapchat 2. Pretty Girl 3. Danger Zone 4. Where You Want 5. Whine 6. Tugende 7. Milele
EP imesukwa na watayarishaji mahiri akiwemo Signbeats, Alkeys, Gachi B, Twayjustis na Slickwidit, huku David Rotimi akifanya mixing na mastering.
Itaré amesema lengo lake ni kutengeneza muziki unaogusa, unaoeneza upendo na kuonyesha toleo bora zaidi la wasanii wapya wa kizazi hiki. Akiwatia moyo mashabiki, alimaliza kwa utani:
“Now go and acquire noise complaints from blasting Itaré too loud.”
Kwa EP hii, Itaré anajiweka rasmi kwenye ramani ya muziki wa kisasa wa Tanzania, akiwa na mwonekano, sauti na kasi ya kuwa miongoni mwa sura mpya za Bongo Fleva.