Msanii chipukizi anayezidi kuteka masikio ya mashabiki wa Bongo Fleva, Itaré, ametoa ujumbe wenye kugusa moyo kuelekea kwa mashabiki wake, huku  akianza kwa kuwaombea amani, utulivu na ustawi kwa Tanzania.
Katika ujumbe huo, Itare ameeleza kuwa amekuwa akitafakari kwa kina kuhusu muda ambao nchi inapitia, bila kutaka kuonekana asiyejua yanayoendelea.
Hata hivyo, amekiri kutambua kwamba muziki ni mkusanyiko wa hisia, na ni katika nyakati kama hizi sanaa ya muziki ina nafasi ya kuleta matumaini, faraja na uponyaji.
Itaré amesema matumaini yake ni kwamba EP yake mpya italeta mwanga mpya wa tumaini kwa kizazi cha sasa na kijacho kazi itakayosaidia Watanzania kujisimamia, kujieleza, na kuwakilisha utambulisho wao duniani kwa uhakika zaidi.
EP hiyo inatarajiwa kutoka tarehe 21 Novemba 2025, na Itaré amewahimiza mashabiki kuanza kufanya pre–order, akisisitiza lengo lake la kuifanya kuwa moja ya kazi zitakazoacha alama kwenye muziki wa Tanzania.
Kwa ujumbe huu, mashabiki wake wamepata picha ya msanii mwenye maono, mwenye kujali taifa lake, na anayeamini katika nguvu ya muziki kama tiba ya kiroho na kijamii.