
Muimbaji na muigizaji Jennifer Lopez ameonyesha kushangazwa na baadhi ya watu ambao hawafurahii uteuzi wake kama msanii atakayeperform kwenye Super Bowl LX Halftime Show.
Akizungumza katika kipindi cha Today Show siku ya Jumatatu, J. Lo alishangaa baada ya kuulizwa kuhusu mjadala unaoendelea mtandaoni.
Lopez amesema kuwa muziki wa Bad Bunny unavuka mipaka ya lugha na kwamba amefanya kitu ambacho wasanii wachache sana wamefanikiwa kufanya.
Bad Bunny, ambaye alitumbuiza pamoja na J. Lo na Shakira kwenye Super Bowl ya 2020, ametangazwa rasmi kuwa staa wa Halftime Show ya mwaka 2026 itakayofanyika Februari 8 katika uwanja wa Levi’s Stadium, California.
Hata hivyo, tangazo hilo limezua mjadala mkubwa nchini Marekani, hasa baada ya taarifa kwamba idara ya ICE (Immigration and Customs Enforcement) itapeleka maafisa wake kwenye tamasha hilo. Wawakilishi wa idara hiyo wamesema watakabiliana na watu wasiokuwa na vibali vya ukaaji nchini humo.
Kwa upande wake, Bad Bunny alijibu kwa utani katika kipindi cha Saturday Night Live (SNL), akisema “Ninafuraha sana, na nafikiri kila mtu ana furaha juu ya hili”.
Wakati mjadala ukiendelea, Jennifer Lopez anajiandaa na filamu yake mpya “Kiss of the Spider Woman,” inayotarajiwa kutoka Ijumaa hii.
Lo amesimama upande wa Bad Bunny, akisema muziki wake ni wa dunia nzima sio wa lugha au taifa fulani na anastahili kabisa heshima ya kuongoza jukwaa la Super Bowl.