Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge Ngara, Severin Niwemugizi, ametoa wito kwa jamii na wadau mbalimbali kushirikiana kurejesha umoja wa kitaifa kwa kukabiliana na changamoto zilizosababisha migawanyiko, hususan baada ya matukio ya Oktoba 29 mwaka 2025.
Askofu Niwemugizi ameyasema hayo leo January 12,2026 wakati wa ufunguzi wa vipindi vya redio kwa mwaka huu na uzinduzi wa kaulimbiu ya mwaka kwa radio nayosema “Aminia”.

Amesisitiza kuwa kurejesha mshikamano wa kitaifa kunahitaji utashi kutoka pande zote, huku akibainisha kuwa vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika kuunganisha jamii kwa kuwa vinaaminiwa na wananchi
Aidha, Askofu Niwemugizi ameipongeza Radio Kwizera kwa kuja na kaulimbiu ya “2026 Aminia”, akisema inahamasisha imani, matumaini na kutokata tamaa.