
Na David Mwaluseke- Ngara, Kagera
Katika kuadhimisha miaka 64 ya Jeshi la Magereza Tanzania Bara baada ya Uhuru, Jeshi hilo wilayani Ngara mkoani Kagera limeshiriki matendo ya kijamii katika hospitali ya Nyamiaga wilayani humo.
Ambapo matendo hayo ni pamoja na kuchangia damu, kufanya usafi wa mazingira na kutoa misaada kwa wagonjwa katika hospitali ya Nyamiaga.
Awali Mrakibu wa Jeshi la Magereza wilayani Ngara Moses Sebastian ameeleza kuwa maadhimisho hayo ni kufuatia maelekezo ya Kamishina wa jeshi la Magereza nchini kuruhusu kufanyika ngazi ya wilaya.
Afisa Tarafa ya Nyamiaga Bw. Jawadu Yusuph akimwakilisha Mkuu wa wilaya amesema ni vyema jamii ikaigamatendo ya kijamii kama mabavyo jeshi la magereza limeshiriki.
Maadhimisho ya miaka 64 ya Jeshi la Magereza Kitaifa yamezinduliwa leo na yatahitimishwa Agosti 26, 2025 huku yakiongozwa na kaulimbiu isemayo Ushirikiano wa Magereza na Jamii kwa urekebishaji wenye tija.