
Msanii wa muziki wa Injili, Joel Lwaga, ameendelea kufungua njia kwa muziki wa Kikristo baada ya kuachia wimbo wake mpya uitwao ‘Saa Hii’ chini ya ‘Empire’, kampuni kubwa ya usimamizi na usambazaji wa muziki yenye makao yake makuu Marekani na tawi barani Afrika.
Meneja na pia mtayarishaji wa nyimbo za Joel Lwaga, @allanepyuza ameeleza kuwa dili hili limekuja wakati sahihi ambapo timu yao ilikuwa ikitafuta ushirikiano wa kukuza soko la muziki wa Injili kimataifa.
Kwa hatua hii, Joel Lwaga anakuwa msanii wa kwanza wa Injili kutoka Afrika Mashariki kusaini mkataba na Empire, hatua inayotafsiriwa kama mlango mpya wa kuinua hadhi ya muziki wa Injili kutoka kanda hii kwenye majukwaa ya kimataifa.