Rapa mkongwe Joh Makini ameweka wazi msimamo wake kuhusu nani ni G.O.A.T kwenye game ya rap Tanzania.
Joh Makini amesema wazi kuwa tangu aanze muziki, hakuna rapa wa kizazi chake anayeweza kulinganishwa naye katika uandishi na ubora wa kazi.
Akizungumzia line yake maarufu kwenye wimbo wa Weusi, Hii hapa aliposema “nimefungua bucha nachinja magoat”, Joh Makini alifafanua kuwa maneno hayo haya kumlenga Young Lunya, bali yalikuwa ni tambo za kishairi kuonyesha ubabe wake kwenye rap.
Hata hivyo, ameongeza kuwa anamkubali Young Lunya kama rapa mwenye kipaji kikubwa, lakini bado hajaifikia hadhi ya kuwa bora wa muda wote (Greatest Of All Time) mpaka atakapokuwa na muendelezo wa kazi bora zaidi.