Msanii wa Bongo Fleva Juma Jux anatarajia kuandika historia tarehe 18 Desemba mwaka huu kwa kuwa msanii wa kwanza kutoka Tanzania kufanya tamasha lake binafsi nchini Nigeria.
Muimbaji huyo, ambaye tangu kufunga ndoa na Mnaijeria Priscilla, amekuwa kipenzi cha mashabiki wengi wa Naija, ameshare video ya tangazo la show hiyo akielezea furaha na shukrani zake kwa mapokezi mazuri anayoyapata nchini humo.
Akiandika kupitia ukurasa wake wa Instagram, Jux amesema: “Upendo na sapoti ambayo ninyi nyote mmenionyesha umekuwa wa ajabu sana! Najisikia kama niko nyumbani hapa Nigeria. Kila jiji lina mdundo wake, lakini Lagos lina roho. TAREHE 18 DESEMBA, tunakuja kwa ukubwa tukileta upendo wote, maisha, na urithi pamoja! Kutoka Tanzania hadi Nigeria, moja kwa moja.”
Muimbaji huyo ameongeza, Juma Jux in Lagos si tukio la muziki pekee bali ni mkutano wa kifamilia unaounganisha watu kupitia upendo na positive vibes.
Kwenye video ya promo hiyo, mke wake Priscilla, mama mkwe wake Iyabo Ojo, pamoja na mastaa kadhaa wa Nigeria wameonekana.