
Kamati ya ulinzi na Usalama Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera jumatatu ya mei 19, 2025 imekamata kahawa mbichi ikiwa imeanikwa katika Kijiji cha Bihanga Kata ya Burungura ikidhaniwa kuwa ni mali ya wizi huku mmiliki wa kahawa hizo akitokomea kusiko julikana.
Mkuu wa Wilaya ya Muleba Dkt. Abel Nyamahanga amesema kuwa kahawa hizo zitataifishwa na kuagiza mmiliki kujitokeza mara moja kabla ya jeshi la Polisi halijaanza kumtafuta.
Dkt. Nyamahanga amesema kwa sasa katika Wilaya hiyo hairuhusiwi mtu yeyote kuchuma kahawa mbichi, kuisafirisha kinyume na utaratibu pamoja na kuianika chini na kupolekea kuiharibu ubora na atakayebainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
Bw. Alex Mathias ni Mwenyekiti Kijiji cha Bihanga amesema watahakikisha wanasimamia swala la Kahawa za magendo kutokana pamekuwepo na baadhi ya watu wakilangua kahawa mbichi kwa wakulima ikiwa bado ipo shambani ambayo ni kinyume na utaratibu.