
Na Zawadi Bashemela- Kigali, Rwanda
Rais wa mabaraza ya maaskofu wa Kanisa Katoliki Barani Afrika Kardinali Fridolaa Ambongosha amesema Kanisa la Afrika linatakiwa kuwa chanzo cha Amani, Upendo na Maridhiano ili kumaliza changamoto zilizopo katika jamii inayolihudumia.
Kardinali Ambongosha ametoa wito huo wakati akifungua rasmi mkutano wa 20 wa mabaraza ya maaskofu Afrika na Madagaska SECAM unaofanyika kwa Kigali nchini Rwanda.
Amesema kuwa Bara la Afrika kwa Sasa linakabiliwa na changamoto ya Vita na njaa miongoni mwa watu wake , hivyo kuna haja ya kanisa kuja na suluhisho la pamoja kwa viongozi viongozi wa Afrika kuacha kuwa watawala na badala yake kuwasaidia wanaopitia mazingira magumu.
Naye Waziri Mkuu wa Rwanda akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo kwa niaba ya rais Paulo Kagame amesema serikali nchini humo inautambua mchango wa Kanisa Katoliki katika sekta za afya, elimu na mazingira na kwamba serikali peke yake haiwezi kutekeleza yote bila mchango wa wadau wa maendeleo.
Mkutano wa 20 wa mabaraza ya maaskofu Barani Afrika na Madagaska uliowakutanisha washiriki 250 unaofanyika kwa siku nne kuanzia July 31, 2025 na unatarajiwa kukalizika August 03, 2025 ukiwa na kauli mbiu Kristo chanzo Cha Tumaini, Maridhiano na Amani.
Washiriki wa mkutano mkuu wa 20 wa mabaraza ya maaskofu wa Kanisa Katoliki Bara la Afrika na Madagaska unaofanyika jijini Kigali nchini Rwanda, uliowashirikisha washiriki 250.
Kauli mbiu ya mkutano huu ni Kristo chanzo Cha Tumaini, Maridhiano na Amani.