
TOPSHOT - Tanzania's main opposition leader Tundu Lissu (2nd L) gestures as he enters the court room at Kisutu magistrate's court in Dar es Salaam on May 19, 2025. Tanzanian opposition leader Tundu Lissu appeared in court on May 19, 2025 for his latest hearing in a treason trial in which he faces a potential death penalty. (Photo by ERICKY BONIPHACE / AFP) (Photo by ERICKY BONIPHACE/AFP via Getty Images)
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu imeendelea leo, katika Mahakama kuu Masijala Ndogo ya Dares Salaam kwa hatua ya kutolewa uamzi mdogo wa mapingamizi yaliyowasilishwa na Lisu dhidi ya Jamhuri.
Mapigamizi yaliyowasilishwa na Lisu ni la uhalali wa hati ya mashtaka dhidi yake, kulindwa kwa mashahidi dhdi ya kesi ya uhaini inayomkabili ambayo alidai hawakufichwa kama inavyotakiwa.
Mahakama kupitia jopo la Majaji watatu (3) wakiongozwa na Jaji Danstan Ndunguru wanaosikiliza kesi hiyo wametupilia mbali mapingamizi hayo, na Lisu amesomewa maelezo ya awali na kesi hiyo imehairishwa hadi Oktoba 06.2025 itakapoanza kusikilizwa rasmi.
Mwenyekiti huyo wa CHADEMA anaendelea na shauri hilo wakati vyama vingine vya siasa vikiendelea na Kampeni zake kuelekea uchagzui mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu, CHADEMA kikiwa ndicho chama pekee hakishiriki uchaguzi huo.