
Kampuni ya Bankiis imeibua tuhuma nzito dhidi ya msanii wa Nigeria, Kizz Daniel, ikiwatahadharisha waandaaji wa matamasha wasimchukue kutokana na kile kinachodaiwa kuwa tabia ya kutojitokeza kwenye shows na kusababisha hasara kubwa.
Kupitia ukurasa wao wa Instagram, Bankiis wamesema Kizz Daniel amekuwa akiacha promoters wakiwa hoi na mashabiki wakiwa wamekatishwa tamaa, huku wakisisitiza kuwa hana mashabiki wa kutosha kwa sasa kuleta faida inayotarajiwa.
Aidha, walimtuhumu kwa vitendo vya “utapeli,” na kutoa wito wa kumaliza mwenendo huo, huku pia wakilaumu promoters wa diaspora, hasa barani Ulaya, kwa kupandisha gharama za wasanii kupita kiasi na kuharibu soko.
Hali hii imezua gumzo mtandaoni, huku wadau wa muziki wakisubiri kuona majibu ya Kizz Daniel kuhusu madai haya.